U-Tena Youth Organization
  • intro
  • Karibu
  • Home
  • Programs
  • Projects
    • Education Projects
    • Health Projects
    • Youth Friendly Services
    • Livelihood Projects
    • Performing Arts
    • Old Projects
    • Completed Projects >
      • Jichanue- SRHR Project
      • Time is Now! Non Communicable Diseases Project
      • Teen Mothers Project
      • Education (ALOT Change)
      • KUZA (SRH and Livelihood)
      • IMARISHA MAISHA (Health)
      • Selfie- HIV Project
      • Sanitation
  • Our Team
  • About Us
  • What we do
  • Get Involved
    • Apply Now
  • Contact and Address
  • Events
    • Upcoming Events
    • International Conferences
  • Media
    • Photo Gallery
    • Pixieset of U-Tena
  • Blogs
  • Jobs
  • Community Conference
Donate

Utu na Ubinadamu

utu na ubinadamu

15/10/2020

0 Comments

 
Picture
Nimeona mengi, nimeona wengi, nimeona vingi na mashirika mengi yaliyofutika akilini na moyoni mwangu, lakini shirika la U-TENA, ni zaidi yao yote.
Nikisikia U-TENA, maana ya utu na ubinadamu husawirika na kujidhihirisha kuhalisia. Hili ni shirika lililojitolea kwa udi na uvumba kuwasaidia wenye hadhi ya chini kwenye haya maeneo ya vitongoji duni vya Mukuru, Viwandani na Korogosho, hakika si dogo.
Ukidhani ni majigambo, karibu kwenye tamasha, hafla na mikutano ya wazazi, wanafunzi na wanaviwandani ili ukapate uhondo wa mazuri wanayofanyiwa na U-TENA. Katika mkutano wa hivi majuzi, nilipata kusikia mwenyewe kutoka kwa mzazi mmoja alivyosimama na kusifia mwanawe alivyokuwa na utundu kabla ya kuingia U-TENA na kuishia kubadilika kabisa kihulka baada ya kupata mafunzo ya life skills na counselling kwenye mradi wa A LOT-change, huku mwingine akishukuru alivyojifunza jinsi ya kuzungumza na mwanawe na kumnasihi na kumpa mawaidha ya kujiendeleza na kuwajibika kupitia mradi wa nasaha bora kwa wazazi (parental counselling). Mwingine naye alisimama na kusifia mwanawe alivyofaidika na mradi wa ufadhili wa masomo (scholarship) kwa kumlipia mwanawe elfu ishirini pamoja na manufaa mengi tu yaliyosemwa. Mwisho wa hafla ilikuwa ni tabasamu huku wazazi wakienda nyumbani na maziwa na mkate kama kiburudisho baada ya mkutano.
Ni mengi sana mazuri ya UTENA ningesema, ila hili la kuwafaa wanaviwandani wakati huu wa tandavu la Corona ni kuu zaidi. Kuna ule msaada wa chakula uliowafaidi wengi wasiojiweza Viwandani. Kisha mradi huu wa kuwafaa wanakidato cha tatu na nne katika durusudurusu zao za kujitayarisha kuukalia mtihani wao wa mwisho wa K.C.S.E, lilikuwa jambo kuu sana kwao.
Kama mwalimu wa Lugha kwenye mradi huu wa Tujifunze, hakika niliuona ukiwa wa manufaa anuwai. Binafsi nilivutiwa na nafasi hii ya kuona wanafunzi wakijitokeza zaidi ya walivyotarajiwa, wakiwa tayari kabisa kusoma. Masomo yalikuwa machangamfu, maswali nayo mengi yaliyonichachawiza kiasi cha kunifanya kujikuna kichwa na hata kuishia kufanya utafiti kutafuta majibu. Hali hii haswa, ilisababishwa na mseto na mchanganyiko wa wanafunzi kutoka shule nyingi, tofauti, za hadhi ya juu na chini, kitaifa na hata za vitongojini, wote walijumuika pamoja na kujifunza kutoka kwa wenzao kama ndugu. Ningependekeza mradi huu adimu uendelee maana una manufaa mengi kwa kizazi hiki na hata vizazi vijavyo. Elimu ni akiba madhuuti ya kesho, na ikiwa wanavitongoji duni wataishia kuelimika, basi akilimali hizi zitabadili haya maeneo ya vitongoji duni kuishia kuwa maeneo ya makasri ya wenye uwezo na hekima.
Nashukuru sana kwa U-TENA kunipa fursa hii ya kufanya kazi nao na itakuwa furaha yangu kufanya nao kazi hata zaidi. U-TENA, endeleeni na juhudi hizi za kuwafaa wanavitongoji duni na msambaze mazuri haya kote nchini na hata nchi za nje. Nawatakia fanaka katika shughuli hizi zenu zote sasa na hata milele.

0 Comments

    Author: ​​Igunza Mwanatunzi

    ​Igunza Mwanatunzi ni mwalimu wa Kiswahili na dini. Vilevile ni mwandishi wa Makala ya Kiswahili. Ameandika Riwaya ya ‘Mateso ya Manoti’ na ‘Binti Wema’. Vilevile, ameandika hadithi fupi nyingi zikiwemo; ‘Ushindi wa Ushindi’, ‘Wakili Gumu Mui’ na ‘Pingu za Pingamizi’ pamoja na hadithi zingine nyingi kwenye mikusanyiko tofauti. Ameandika Mashairi mengi yaliyowahi kuchapishwa yakiwemo yaliyochapishwa na gazeti la Taifa Leo- Tuepushie Corona tarehe 3, Mei 2020 na Tusafishe Ufisadi, tarehe 28, Juni 2020 pamoja na Makala mengine mengi.
    Vilevile ni mwalimu na Mshauri (Mentor) kwenye shirika la U-TENA.

    Archives

    October 2020

    Categories

    All

    RSS Feed

    Subscribe to our newsletter:

Subscribe to Newsletter

Home

About Us

What We Do

Current Projects

Contacts

Blogs     Completed Projects     Our Team      Events     Media     Photo Gallery     Get Involved     International Conferences
  • intro
  • Karibu
  • Home
  • Programs
  • Projects
    • Education Projects
    • Health Projects
    • Youth Friendly Services
    • Livelihood Projects
    • Performing Arts
    • Old Projects
    • Completed Projects >
      • Jichanue- SRHR Project
      • Time is Now! Non Communicable Diseases Project
      • Teen Mothers Project
      • Education (ALOT Change)
      • KUZA (SRH and Livelihood)
      • IMARISHA MAISHA (Health)
      • Selfie- HIV Project
      • Sanitation
  • Our Team
  • About Us
  • What we do
  • Get Involved
    • Apply Now
  • Contact and Address
  • Events
    • Upcoming Events
    • International Conferences
  • Media
    • Photo Gallery
    • Pixieset of U-Tena
  • Blogs
  • Jobs
  • Community Conference